Mwongozo wa kufundishia wafanyabiashara wa maziwa Afrika Mashariki MODULI 4 Biashara ya maziwa bora FEBRUARI 2011 KShs 200/= FEBRUARI 2011 MODULI 4 Biashara ya maziwa bora Mwongozo wa kufundishia wafanyabiashara wa maziwa Afrika Mashariki BIASHARA YA MAZIWA BORA ii Wachangiaji Isha Muzira (Uganda) Michel Ngarambe (Rwanda) Obed Ndankuu (Tanzania) Philip K Cherono (Kenya) Dairy Development Authority S.L.P. 34006 Kampala UGANDA Ministry of Agriculture (MINAGRI) S.L.P. 621 Kigali RWANDA Tanzania Dairy Board S.L.P. 38456 Dar es Salaam TANZANIA Kenya Dairy Board S.L.P. 30406 GPO 00100 Nairobi KENYA iii MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 ? Association for Strengthening Agricultural Research in Eastern and Central Africa (ASARECA), 2011. Haki zote zimehifadhiwa. Sehemu ya kitabu hiki inaweza kutumika bila idhini ya waandishi iwapo haitumiki kibiashara na ikiwa ASARECA watatambuliwa kama rejea. Wachangiaji: Isha Muzira Michel Ngarambe Obed Ndankuu Philip K Cherono Uhakiki na uhariri: Tezira A. Lore, ILRI (International Livestock Research Institute), Kenya Lusato R. Kurwijila, Sokoine University of Agriculture, Tanzania Amos Omore, ILRI (International Livestock Research Institute), Kenya Upangaji na michoro: Lilian Ohayo Mchapishaji: Regal Press Kenya Limited, Nairobi ISBN: 92?9146?252?7 Correct citation: Lore, T.A., Kurwijila, L.R. na Omore, A. (wahariri). 2011. Biashara ya maziwa bora: Mwongozo wa kufundishia wafanyabiashara wa maziwa Afrika Mashariki (Imetafsiriwa na Tanzania Dairy Board). ILRI (International Livestock Research Institute), Nairobi, Kenya. (Toleo ya asili 2006, Hygienic milk trading: A training guide for small-scale milk traders in Eastern Africa). BIASHARA YA MAZIWA BORA iv v MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 Yaliyomo SHUKURANI vi DIBAJI viii UZALISHAJI BORA WA MAZIWA 1 Mambo muhimu yanayochangia ubora wa maziwa 1 Afya ya mnyama na kiwele 2 Ukamuaji bora 2 UTUNZAJI BORA WA MAZIWA 5 Nini husababisha maziwa kuharibika? 5 Vifaa vya kuhifadhia maziwa 6 Matumizi salama ya sabuni za kuoshea 7 Utaratibu wa kusafi sha vyombo vya kuhifadhi maziwa 7 VIPIMO VYA MSINGI VYA KUHAKIKI UBORA WA MAZIWA 9 Kipimo cha kuangalia na kunusa 9 Kipimo cha kuchemsha 10 Kipimo cha alkoholi 11 Kipimo cha laktomita 12 UTUNZAJI NA UHIFADHI BORA WA MAZIWA 14 Vyombo vinavyoruhusiwa kwa kutunzia maziwa 14 Mbinu sahihi za kuhifadhi maziwa 14 Usafi na utunzaji katika kituo cha kuuzia maziwa 15 KIAMBATISHO 18 Mtaala wa mafunzo na ustadi kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa maziwa BIASHARA YA MAZIWA BORA vi Shukurani Asasi za Dairy Development Authority (Uganda), Kenya Dairy Board, Rwanda Animal Resources Development Authority na Tanzania Dairy Board zinatoa shukurani kwa taasisi na watu binafsi wafuatao kwa kufanikisha uandaaji wa mwongozo huu wa mafunzo: ? Wataalamu wa kitaifa wa asasi hizo walioshiriki katika kukusanya taarifa zilizotumika kulinganisha mitaala ya mafunzo na kuandaa mwongozo huu: ? Bw. Isha Muzira (Uganda) ? Dkt. Philip K Cherono (Kenya) ? Dkt. Michel Ngarambe (Rwanda) ? Bw. Obed Ndankuu (Tanzania) ? Asasi ya Association for Strengthening Agricultural Research in Eastern and Central Africa (ASARECA) kupitia Programme for Agricultural Policy Analysis (PAAP) kwa kugharamia na awamu mbili za mradi wa Kulinganisha na kuoanisha sera, viwango na kanuni katika tasnia ya maziwa Afrika Mashariki 2002 hadi 2005. ? Asasi ya International Livestock Research Institute (ILRI) kupitia utafi ti wake wenye dhamira ya uzalishaji wa maziwa unaolenga soko. ? Profesa Lusato Kurwijila wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro, Tanzania kwa kuchangia utalaamu na ujuzi wake kwa tasnia ya maziwa katika bara la Afrika ambao ulikuwa muhimu katika kuandaa mtaala na mwongozo huu. ? Dkt. Amos Omore (ILRI) kwa kuratibu kazi ya wataalam na kuwezesha majadiliano na kubadilishana uzoefu ili kuongeza ubora wa maziwa yanayouzwa katika sekta isiyo rasmi. vii MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 ? Bi. Tezira Lore (ILRI) kwa kuhariri, kupitia na kusanifu mpangilio wa mwongozo huu. ? Bi. Lilian Ohayo kwa kutoa michoro na vielelezo. ? Asasi ya US Agency for International Development (USAID), Regional Economic Development Services Offi ce for East and Southern Africa, kwa kugharamia Ni matumaini yetu kuwa matumizi ya mwongozo huu katika programu za mafunzo zitatumika kuendeleza ubora wa maziwa katika mfumo mzima wa masoko ya maziwa na kutoa fursa za kuongeza kipato kwa waliohusika. Tunatarajia kuendeleza ushirikiano na asasi hizo kadiri tunavyoongeza juhudi katika kuimarisha tasnia ya maziwa na biashara baina ya nchi na nchi katika kanda ya Afrika Mashariki. BIASHARA YA MAZIWA BORA viii Dibaji Kama mfanyabiashara mdogomdogo wa maziwa, unafahamu vyema jinsi maziwa yanavyoweza kuharibika haraka kama hayatatunzwa na huhifadhiwa vizuri. Hivyo basi, ni muhimu kuwa na uelewa wa kutosha na stadi zitakazokuwezesha kuzingatia misingi ya ubora wa maziwa wakati unapohudumia na kwenda kuyauza kwa wateja. Hii itasaidia kuzuia hasara zisizo za lazima kutokana na kuharibika kwa maziwa na itakuwezesha kuongeza faida. Kwa kuzingatia hayo mwongozo ufuatao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya mamlaka zinazosimamia tasnia ya maziwa za Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda; Asasi za Association for Strengthening Agricultural Research in Eastern and Central Africa (ASARECA) kupitia Programme for Agricultural Policy Analysis (PAAP) na International Livestock Research Institute (ILRI). Mwongozo huu umetengenezwa ili kukupa misingi ya uelewa biashara na usafi rishaji bora wa maziwa. Madhumuni ya mwongozo huu ni kukusaidia kupata misingi ya uelewa na stadi katika maeneo yafuatayo: ? Uzalishaji bora wa maziwa ? Kuhudumia maziwa katika hali ya usafi na salama ? Vipimo vya msingi vya kuhakiki ubora wa maziwa ? Utunzaji, uhifadhi na biashara bora wa maziwa Mwongozo huu umeandaliwa ili kutumika vituoni kwa vipindi vya saa 2-3 kwa siku, katika eneo muafaka. Baada ya mafunzo, utafanya majaribio ya nadharia na vitendo kupima uelewa na umahiri wako katika njia bora za kuhudumia maziwa katika hali ya usafi na salama. Kama utafaulu, utatuzwa cheti cha misingi cha biashara ya maziwa bora. Ni lazima upitie mafunzo haya kabla ya kupata leseni inayotolewa na mamlaka za kitaifa zinazosimamia tasnia ya maziwa kama muuzaji mdogomdogo wa maziwa. ix MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 Kuna miongozo ya mafunzo kama hii ya kufundishia wafugaji, wakusanyaji, wasafi rishaji na wasindikaji ambayo inaleta umahiri katika utunzaji na usindikaji bora wa maziwa. Mwongozo wa misingi ya uendeshaji biashara ya maziwa na masoko siyo kigezo cha kupata leseni ya kuendesha biashara ya maziwa lakini ni hiyari kwa wale wanaopenda kupata mafunzo ya msingi katika eneo hili. Kama wasimamizi wa tasnia ya maziwa Afrika Mashariki, tunashauri mwongozo huu utumike kwa mafunzo, kuwatambua na kuwathibitisha wafanyabiashara wadogowadogo wa maziwa. Machira Gichohi Mkurugenzi Mtendaji Kenya Dairy Board Theogene Rutagwenda Mkurugenzi Mtendaji Rwanda Animal Resources Development Authority Charles Mutagwaba Kaimu Msajili na Ofi sa Mtendaji Mkuu Tanzania Dairy Board Nathan Twinamasiko Mkurugenzi Mtendaji Dairy Development Authority, Uganda Nairobi, Februari 2011 BIASHARA YA MAZIWA BORA x 1 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 UZALISHAJI BORA WA MAZIWA Ni muhimu kwa mfanyabiashara mdogomdogo wa maziwa kuelewa kuwa maziwa yasipohudumiwa katika hali ya usafi kutoka kwa mfugaji, ubora wake utapungua na hatimaye kukataliwa na wateja. Kwa sababu hiyo, sehemu hii ya uzalishaji bora wa maziwa imewekwa ili kusaidia kuelewa baadhi ya mambo muhimu katika ngazi ya mfugaji yanayoweza kuharibu ubora wa maziwa kwenye hatua zingine zinazofuata. Maziwa yanayokamuliwa kutoka kwenye ng?ombe mwenye afya yanakuwa na bakteria wachache sana. Uchafu unaingiza bakteria wanaosababisha maziwa kuharibika haraka. Ili kuhakikisha maziwa yanaendelea kuwa freshi kwa muda mrefu zaidi unahitaji usafi wa ukamuaji na utunzaji wa maziwa. Mambo muhimu yanayochangia ubora wa maziwa Ulishaji Mnyama aliyelishwa vizuri na kupata maji ya kutosha huzalisha maziwa mengi yenye virutubisho vya kutosha. Iwapo ng?ombe hatalishwa majani kidogo na chakula chenye wanga mwingi, kiasi cha mafuta kwenye maziwa kinaweza kushuka chini ya asilimia 2.5. Hivyo, uwiano mzuri wa majani na chakula cha ziada ni muhimu. Unaweza kumlisha ng?ombe chakula cha ziada lakini hakikisha kuna uwiano mzuri. Usimlishe silaji ng?ombe wakati wa kukamua au muda mfupi kabla ya kukamua kwa vile yatachukua ladha ya silaji. Inashauriwa kuwa ng?ombe apewe silaji saa mbili kabla ya kukamuliwa. Afya ya ng?ombe Ng?ombe asiye na afya hali chakula vizuri na huzalisha maziwa kidogo na yasiyo na ubora unaotakiwa. Wakati wote ng?ombe anatakiwa kuwa msafi na mwenye afya kwa sababu wanyama wagonjwa hueneza magonjwa kama vile kifua kikuu na ugonjwa wa Hakikisha ng?ombe wako ana afya na amelishwa vizuri BIASHARA YA MAZIWA BORA 2 kutupa mimba pamoja na homa za vipindi kwa watumiaji wa maziwa. Ukihisi kuwa ng?ombe ni mgonjwa, wasiliana na mhudumu wa afya ya mifugo mara moja. Usiuze wala usinywe maziwa yaliyokamuliwa kutoka kwa ng?ombe aliyetibiwa kwa dawa ya kiuavijasumu (antibiotics) hadi muda uliopendekezwa utakapokwisha. Afya ya mnyama na kiwele Magonjwa ya kuambukiza baina ya wanyama na binadamu Binadamu anaweza kuambukizwa kifua kikuu na ugonjwa wa kutupa mimba na homa ya vipindi kutoka kwa mnyama kwa kutumia maziwa. Taarifa za ng?ombe wanaoumwa magonjwa kama hayo inabidi zipelekwe kwa daktari wa mifugo ambaye atachukua hatua zinazofaa. Wafugaji wanahimizwa kuchanja mifugo yao dhidi ya ugonjwa wa kutupa mimba. Pia uchunguzi wa magonjwa yanayoambukiza unatakiwa ufanyike mara kwa mara na endapo yatabainika kuwepo yatibiwe mara moja. Ugonjwa wa kuvimba kiwele Ugonjwa wa kuvimba kiwele husababishwa na bakteria mbalimbali. Bakteria hao huweza kuingia kwenye maziwa na hivyo kuweza kusababisha ugonjwa kwa mlaji. Kwa sababu hiyo maziwa kutoka ng?ombe anayeugua ugonjwa huu hayafai kwa matumizi ya binadamu. Kuzingatia usafi na utaratibu wa ukamuaji ni njia bora ya kudhibiti ugonjwa wa kuvimba kiwele. Nywele katika kiwele zinapaswa kuwa fupi au zipunguzwe inapobidi. Hakikisha ng?ombe wote wanaougua ugonjwa wa kuvimba kiwele wanatibiwa na daktari wa mifugo. Usiuze wala usinywe maziwa yaliyokamuliwa kutoka kwa ng?ombe aliyetibiwa kwa dawa ya kiuavijasumu hadi muda uliopendekezwa utakapokwisha kwa sababu zinaweza kusababisha mzio na usugu wa dawa mwilini kwa binadamu. Ukamuaji bora Kumbuka kuwa udhibiti wa ubora wa maziwa huanzia kwa mfugaji. Kwa kufanya hivyo, utapunguza kuwepo kwa bakteria wanaoharibu maziwa na kusababisha magonjwa. Ili kuhakikisha ubora na kulinda afya ya watumiaji huna budi kuzingatia utaratibu mzuri wa ukamuaji kama ifuatavyo: ? Hakikisha ng?ombe ni wenye afya na wasafi . 3 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 ? Mazingira ya kukamulia yawe safi , yasiwe na vumbi wala matope. ? Usikamue maziwa ikiwa unaumwa magonjwa ya kuambukiza kama kuhara au homa ya matumbo hadi utakapotibiwa na kupona. ? Usiyachanganye dang?a (maziwa yanayokamuliwa siku saba za mwanzo baada ya ng?ombe kuzaa) na maziwa ya kawaida. ? Nawa mikono kwa kutumia sabuni na maji safi kabla ya kukamua ? Osha kiwele kwa kutumia kitambaa safi na maji ya uvuguvugu ? Kausha kiwele kwa kutumia kitambaa kikavu na safi ? Kamulia kidogo kwenye kikombe maalum kwanza, chunguza ugonjwa wa kuvimba kiwele kisha mwaga maziwa hayo mbali na eneo la kukamulia hata kama yanaonekana salama ? Tumia vyombo safi vya kukamulia. ? Ng?ombe mwenye ugonjwa wa kuvimba kiwele wakamuliwe mwisho na maziwa yao yamwagwe katika shimo na kufukiwa ? Ng?ombe aliyetibiwa kwa kiuavijasumu, maziwa yake yasiuzwe wala kutumika kwa muda wa siku tatu baada ya matibabu ya mwisho au itakavyoshauriwa na mganga wa mifugo. ? Mara baada ya kukamua chovya chuchu katika dawa maalum (kemikali inayozuia kukua kwa bakteria) ? Wakati wa kukamua, mkamuaji hatakiwi; (a) kuwa na kucha ndefu, (b) kupiga chafya, kutema mate au kukohoa, (c) kuvuta sigara. Nawa mikono kwa kutumia sabuni na maji safi kabla ya kukamua BIASHARA YA MAZIWA BORA 4 ? Baada ya kukamua, chuja maziwa kwa kutumia chujio au kitambaa maalum ili kuondoa uchafu. ? Funika maziwa ili kuzuia uchafu usiingie. ? Hifadhi maziwa sehemu safi yenye baridi. Wakati wa kukamua usi? Funika maziwa ili kuzuia uchafu usiingie ...we na kucha ndefu ...vute sigara ?pige chafya, usiteme mate au kukohoa ? Baada ya kukamua mwondoe ng?ombe katika eneo la kukamulia mara moja. 5 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 UTUNZAJI BORA WA MAZIWA Nini husababisha maziwa kuharibika? Ni muhimu kujua baadhi ya mambo ambayo husababisha maziwa kuharibika ili uweze kuzuia hasara zisizokuwa za lazima. Maziwa yana virutubisho vingi sana. Kwa sababu hiyo, bakteria waharibifu huweza kukua kwa haraka kwenye maziwa. Seli za bakteria huongezeka kwa kugawanyika mara mbili kila mara. Maziwa yakihifadhiwa katika hali ya joto, bakteria huongezeka kwa haraka na kusababisha maziwa kuharibika katika muda mfupi. Kama maziwa yatakuwa na bakteria wengi mwanzoni, yataharibika haraka. 1 2 4 8 16 32?64... Seli za bakteria huongezeka kwa kugawanyika mara mbili kila mara Utunzaji mbaya wa maziwa na uongezaji wa maji au kitu kingine chochote kisicho asili ya maziwa huingiza bakteria wanaoharibu maziwa. Yafuatayo ni miongozo ya kufuata ili kupunguza idadi ya bakteria kwenye maziwa na kuzuia uharibikaji wa maziwa: ? Tumia vyombo vya metali na vilivyo safi kuhifadhia maziwa kila wakati. ? Unapohamisha maziwa kutoka chombo kimoja kwenda chombo kingine, mimina badala ya kuchota. Kuchota kunasababisha kuingiza bakteria waharibifu kwa maziwa. ? Ikiwa unaumwa, usikamue wala usijishughulishe na kazi za maziwa. Pata matibabu hadi hapo daktari atakapokuruhusu kuendelea na shughuli zako. ? Usihifadhi maziwa kwenye joto. ? Usikae na maziwa muda mrefu, yapeleke kwenye kituo cha kukusanyia maziwa mapema. BIASHARA YA MAZIWA BORA 6 Vifaa vya kuhifadhia maziwa ? Mara zote tumia vifaa vilivyothibitishwa kwa matumizi ya maziwa, k.m. alumini, chuma kisichopata kutu au vifaa vya plastiki maalum kwa matumizi ya vyakula ambayo hutumika mara moja tu. Vifaa vya metali vinakubalika zaidi kwa kuwa ni rahisi kusafi shwa na kufi sha vijidudu. ? Usihifadhi maziwa kwenye vyombo vya plastiki ambavyo vimetumika kuhifadhia rangi, madawa na kemikali zingine kwa sababu mabaki yake yanaweza kuweka harufu kwenye maziwa. Kuchota kunasababisha kuingiza bakteria waharibifu Mimina badala ya kuchota Hifadhi maziwa kwenye vyombo vya metali, SIYO vyombo vya plastiki 7 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 Matumizi salama ya sabuni za kuoshea Kuna aina mbalimbali za sabuni ambazo zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kusafi shia mashine na vifaa vya kuhifadhia maziwa. Unaweza kutumia pia sabuni ya kumiminika iliyotengenezwa maalum kwa ajili ya kusafi shia vifaa vya kuhifadhia maziwa yenye uwezo wa kuua bakteria. Suuza vyombo ipasavyo mara baada ya kutumia ili kuondoa mabaki ya sabuni ambayo yanaweza kuchafua maziwa. Hifadhi vizuri sabuni za kuoshea vyombo, kwa vile baadhi huweza kuathiri ngozi ya mwili. Zingatia maelekezo ya watengenezaji kuhusu matumizi sahihi ya sabuni hizo. Utaratibu wa kusafi sha vyombo vya kuhifadhi maziwa Kabla ya kurudia kutumia tena chombo cha maziwa: ? Mara baada ya kuondoa maziwa, suuza chombo kwa maji ya kawaida. ? Sugua vizuri chombo kwa brashi na maji ya uvuguvugu kwa kutumia sabuni. ? Suuza chombo kwa maji safi ? Tumbukiza chombo kwenye maji yanayochemka kwa angalau dakika moja ili kuua vijidudu. Unaweza pia kusuuza kwa kutia maji ya moto kwenye chombo. ? Anika kwenye kichanja safi kwa kupindua chombo kikiwa wazi. Sugua vizuri chombo kwa brashi na maji ya uvuguvugu kwa kutumia sabuni BIASHARA YA MAZIWA BORA 8 AU Tumbukiza chombo kwenye maji yanayochemka angalau kwa dakika moja ili kuua vijidudu Tia maji ya moto kwenye chombo Anika kwenye kichanja safi kwa kupindua chombo kikiwa wazi 9 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 VIPIMO VYA MSINGI VYA KUHAKIKI UBORA WA MAZIWA Kuna vipimo vinne rahisi vya kuhakiki ubora wa maziwa: ? kipimo cha kuangalia na kunusa ? kipimo cha kuchemsha ? kipimo cha alkoholi ? kipimo cha laktomita Vipimo hivi hufanyika kila wakati maziwa yanapofikishwa katika vituo vya kukusanyia maziwa ili kuhakikisha maziwa bora pekee ndiyo yanayopokelewa. Kwa kawaida wakati wa kupima ubora, kiasi kidogo cha maziwa (sampuli) kutoka kwenye kila chombo hupimwa. Maziwa ambayo sampuli yake haikufi kia kiwango kinachotakiwa hukataliwa na ni hasara kwa mfugaji. Kwa hiyo, ni muhimu kushughulikia na kuhifadhi maziwa kwa kuzingatia kanuni za usafi . Utaratibu huu wa upimaji maziwa kama unavyofafanuliwa hapo chini utakusaidia kuelewa na kukubali matokeo ya upimaji. Kipimo cha kuangalia na kunusa Kipimo hiki hufanyika awali kupima ubora wa maziwa kwa kuangalia rangi, mwonekano na harufu. Kipimo hiki ni cha haraka na rahisi kufanyika ili kutambua maziwa yasiyo bora. Kipimo hiki hakihitaji kifaa chochote, ila mpimaji anatakiwa kuwa na uzoefu na uwezo wa kuona na kunusa. Iwapo ubora wa maziwa hauwezi kuthibitishwa kwa kipimo hiki, inabidi vipimo vingine bora zaidi vitumike. Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia ? Funua chombo chenye maziwa ? Nusa mara unapofunua na gundua aina ya harufu iliyomo. Maziwa yenye harufu ya kuchachuka au harufu nyingine yoyote isiyo ya kawaida kama vile rangi au mafuta ya taa yasipokelewe. ? Angalia rangi ya maziwa. Iwapo yana tofauti na rangi ya kawaida ya maziwa, inaashiria ugonjwa wa kuvimba kiwele (wekundu ni damu, njano ni usaha). BIASHARA YA MAZIWA BORA 10 ? Angalia kama kuna uchafu ambayo huashiria kuwa maziwa hayakukamuliwa na kutunzwa katika hali ya usafi . ? Gusa chombo cha maziwa kwa kuangalia joto la maziwa. Hii inaashiria kujua muda uliotumika tangu maziwa yalipokamuliwa (kama hayajapozwa). Joto la maziwa huathiri kipimo cha laktomita. Matokeo Mwonekano na harufu isiyo ya kawaida unaoweza kusababisha maziwa kukataliwa ni kama vifuatavyo: ? Aina ya chakula au harufu ya mazingira ya ukamuaji au utunzaji ? Ng?ombe wanaokaribia kukaushwa ? Harufu ya bakteria ? Harufu ya kemikali au rangi isiyo ya kawaida ? Kuchachuka kupita kiasi Kujitenga kwa mafuta kunaweza kusababishwa na: ? Maziwa ambayo yalipozwa na kisha yakatikiswa sana wakati wa kuyasafi risha ? Kuongeza vitu vingine (yanaweza pia kuonyesha chenga au taka chini ya chombo chenye maziwa) ? Kuchemsha, kama mafuta yameganda Kipimo cha kuchemsha Kipimo hiki ni cha haraka na rahisi. Kinasaidia kugundua maziwa yaliyokaa muda mrefu baada ya kukamuliwa bila kupozwa na hivyo kuanza kuganda, au dang?a ambayo kawaida yana protini nyingi. Maziwa kama hayo hayawezi kustahimili joto wakati wa kuchemsha, hivyo kipimo kitaonyesha matokeo mazuri kwenye maziwa yanayoanza kuganda. Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia na matokeo ? Kwa sekunde chache chemsha kiasi kidogo cha maziwa kwenye kijiko au chombo chochote kinachofaa. 11 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 ? Angalia haraka kama yanaganda ? Maziwa yatakataliwa kama yataganda, yatakuwa na vibonge au chengachenga. Kipimo cha alkoholi Kipimo hiki ni cha haraka na rahisi. Alkoholi maalum inayotumika inaitwa ?ethanoli?. Kipimo hiki ni makini zaidi kwa kutambua maziwa yaliyoanza kuganda na yaliyojaribiwa kwa vipimo hivyo vingine vya awali. Pia kipimo hiki hutambua maziwa yaliyokaa muda mrefu bila kupozwa, dang?a au maziwa kutoka kwenye ng?ombe mwenye ugonjwa wa kuvimba kiwele. Kwa kuwa hiki kipimo ni makini zaidi, maziwa yanayopita kipimo hiki yanaweza kuhifadhiwa kwa saa mbili kabla hayajaharibika. Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia na matokeo ? Tumia bomba la sindano kunyonya kiasi kinacholingana cha maziwa na alkoholi yenye kiwango cha asilimia 70 kisha tia katika neli ya majaribio au testityubu (test tube) au glasi nyeupe (kama kikombe maalum kinachotumika kuwapa dawa watoto). ? Changanya na kutikisa ml. 2 za maziwa na ml. 2 za alkoholi kisha angalia kama maziwa yataganda. ? Iwapo maziwa yataganda, yasipokelewe. AU Kipimo cha kuchemsha BIASHARA YA MAZIWA BORA 12 Kipimo cha laktomita Kipimo hiki kinatumika kugundua kama maziwa yameongezwa maji au vitu vingine. Kuchanganya kitu chochote na maziwa husababisha kuingiza bakteria ambao huharibu maziwa mapema. Uongezaji wa vitu kwenye maziwa ni kukosa uaminifu kwa watumiaji na ni kuvunja sheria. Kipimo cha laktomita kinatumika kwa sababu maziwa yenye 1.026 ? 1.032 g/ml n i mazito zaidi kuliko maji yenye 1.000 g/ml. Kwa hiyo maziwa yakiongezwa maji au vitu vingine, uzito unapungua (kama yamewekwa maji) au unaongezeka (kama yamewekwa vitu vingine vizito). Kama maziwa yameongezwa mafuta (krimu) uzito unapungua. Kifaa kinachotumika kupima uzito wa maziwa kinaitwa laktomita. Laktomita nyingi huanzia kwenye ?0? ikiwa na maana ya uzito wenye 1.000 g/ml mpaka ?40? ikiwa na maana ya uzito wenye 1.040 g/ml . Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia ? Baada ya kukamua acha maziwa kwa angalau dakika 30 ili yafi kie joto la kawaida mathalan, nyuzijoto 20 Sentigredi (20?C). ? Koroga sampuli ya maziwa kisha mimina taratibu kwenye silinda ya kupima yenye ujazo wa ml 200 au chombo chenye kina kirefu kama laktomita. ? Zamisha laktomita taratibu ndani ya maziwa. ? Soma namba ya laktomita usawa wa maziwa. Kipimo cha alkoholi Changanya na kutikisa ml. 2 za maziwa na ml. 2 za alkoholi Iwapo maziwa yataganda, yasipokelewe Maziwa Alkoholi 13 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 Ikiwa joto la maziwa ni tofauti na lile la laktomita (20?C), rekebisha kama ifuatavyo: ? Kwa kila nyuzijoto ya maziwa inayozidi joto la laktomita, ongeza digrii 0.2 (?L) katika kipimo kilichopatikana cha laktomita. ? Kwa kila nyuzijoto ya maziwa inayopungua joto la laktomita, punguza digrii 0.2 (?L) katika kipimo kilichopatikana cha laktomita. ? Angalizo: masahihisho haya hufanyika kwenye vipimo vya laktomita (k.m. 29 badala ya uzito halisi wa 1.029 g/ml). Mifano ya kukokotoa kipimo sahihi cha laktomita inapotokea joto la maziwa linatofautiana na joto la laktomita la nyuzijoto 20 Sentigredi Vifaa vya kupimia uzito wa maziwa Joto la Kipimo Masahihisho Kipimo cha Uzito halisi maziwa cha ?L laktomita g/ml ?C laktomita ?L halisi ?L 17 30.6 - 0.6 30.0 1.030 20 30.0 nil 30.0 1.030 23 29.4 + 0.6 30.0 1.030 Matokeo Iwapo maziwa ni ya kawaida, kipimo cha laktomita kitasoma kati ya digrii 26 na 32. Iwapo kipimo cha laktomita kimo chini ya digrii 26 au zaidi ya digrii 32, maziwa yatakataliwa kwa sababu vipimo hivi vinamaanisha kuwa maziwa yameongezwa maji au vitu vingine. BIASHARA YA MAZIWA BORA 14 UTUNZAJI NA UHIFADHI BORA WA MAZIWA Yafuatayo ni maelekezo ya kuhakikisha maziwa yanakuwa bora wakati wa kutunza na kuhifadhi kwenye kituo chako cha kuuzia: Vyombo vinavyoruhusiwa kwa kutunzia maziwa ? Vyombo vyote vya kutunzia maziwa vinatakiwa kuwa safi na vimetengenezwa kwa kutumia alumini, chuma kisichopata kutu na plastiki maalum. Vyombo hivi ni rahisi kusafi sha. ? Mahali pa kuhifadhia maziwa panatakiwa kuwa safi , pasipokuwa na wadudu, penye hewa na mwanga wa kutosha na ambapo vumbi, mionzi ya jua na mvua haingii. ? Maziwa yasihifadhiwe katika chumba kimoja na mazao ya kilimo (k.m. kabichi, vitunguu, pumba, n.k.) au kemikali kama vile rangi au mafuta ya taa ambavyo hutoa harufu. Mbinu sahihi za kuhifadhi maziwa ? Kwa kuwa maziwa yanaharibika haraka yakiachwa kwenye hali ya joto kwa muda mrefu, yanahitaji kuhifadhiwa kwenye baridi mara baada ya kukamuliwa. Baridi hupunguza kasi ya kuongezeka kwa bakteria waharibifu. Kama huna jokofu au chombo cha kupoza maziwa, hifadhi ndani ya chombo chenye maji baridi au zungushia gunia au blanketi bichi, lakini hakikisha kuwa chombo chenye maziwa kimefunikwa vizuri ili uchafu usiingie ndani. ? Maziwa yanaweza kuchemshwa ili kuua bakteria ila yapozwe haraka katika maji baridi ili yabaki kuwa freshi. 15 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 Usafi na utunzaji katika kituo cha kuuzia maziwa ? Hakikisha kituo chako cha biashara kinakuwa safi wakati wote, bila wadudu na kufanyiwa matengenezo mara kwa mara. ? Wahudumu wote wa kituo cha kuuzia maziwa wawe katika hali ya usafi na wavae mavazi safi na maalum wakati wa kuhudumia maziwa na bidhaa zake. Unaweza kuhifadhi maziwa kwa kuyafunika ... ...ndani ya kabati la baridi la mkaa ...ndani ya beseni au sufuria la maji baridi Chemsha maziwa ili kuua bakteria BIASHARA YA MAZIWA BORA 16 ? Wahudumu wa maziwa wanapaswa kwenda hospitalini kupimwa afya zao mara kwa mara na wataruhusiwa kuhudumia maziwa baada ya kupata cheti kilichothibitishwa na daktari. ? Baada ya kupima maziwa kwenye chombo cha mteja, tundika mjali wa metali wa kupimia ndani ya keni la maziwa ili usichafuke. ? Mara baada ya matumizi, vifaa vyote visafi shwe na kufukizwa mara moja. Kwa maelezo zaidi ya usafi wa vyombo vya kuuzia maziwa, rejea ?Utaratibu wa kusafi sha vyombo vya kuhifadhi maziwa? katika aya za awali za mwongozo huu. Wahudumu wawe wasafi na wavae mavazi safi na maalum 17 MWONGOZO WA KUFUNDISHIA WAFANYABIASHARA WA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI : MODULI 4 KUMBUKA! Kuzingatia kanuni za usafi na utunzaji bora katika biashara ya maziwa ni muhimu kwa kudhibiti ubora na usalama wa maziwa. Kupoza maziwa hufanya maziwa yasiharibike haraka kwani hupunguza kuongezeka kwa bakteria waharibifu. Maziwa yasafi rishwe kwenda kituoni au kiwandani haraka iwezekanavyo ili kuepuka kuharibika. Lakini maziwa ambayo tayari yana bakteria wengi huharibika haraka, hata yakipozwa. Maziwa bora yana bei nzuri na faida kwa biashara yako. BIASHARA YA MAZIWA BORA 18 KIAMBATISHO Mtaala wa mafunzo na ustadi kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa maziwa Mafunzo haya yatafanyika kwa vipindi vya saa 2?3 kwa siku katika eneo la biashara/kituo maalum kwa muda wa wiki 1?2 ili kukamilisha saa 40 za somo. Walengwa Aina ya mafunzo Namna ya mafunzo & mahali Vipindi Wafanyabiashara wadogowadogo wa maziwa Usafi katika biashara ya maziwa Kituoni Uzalishaji wa maziwa Vipengele Malengo (Ustadi unaohitajika) Yaliyomo katika mafunzo Mbinu za ufundishaji/vifaa Tathmini TuzoMuda 1. Uzalishaji bora wa maziwa Wafanyabiashara wadogowadogo wenye uzoefu na ujuzi katika mambo muhimu yanayochangia ubora wa maziwa Mambo muhimu yanayochangia ubora wa maziwa - Ulishaji - Afya ya mnyama - Namna ya ukamuaji Majaribio ya mwisho ya kinadharia kwa kuandika au mazungumzo Majaribio ya mwisho kwa vitendo Faulu au shindwa Saa 1 Mihadhara Majadiliano Maswali & majibu Mbinu shirikishi za kufundisha watu wazima Nadharia Kwa vitendo Afya ya mnyama na kiwele - Magonjwa ya kuambukiza baina ya mnyama na binadamu - Ugonjwa wa kuvimba kiwele Dakika 45 Dakika 45 Saa 2 Ukamuaji bora 2. Kuhudumia maziwa katika hali safi na salama Wafanyabiashara wadogowadogo wenye uzoefu na ujuzi katika kuhudumia maziwa katika hali safi na salama 3. Vipimo vya msingi vya kuhakiki ubora wa maziwa Wafanyabiashara wadogowadogo wenye uzoefu na ujuzi katika vipimo vya msingi vya kuhakiki ubora wa maziwa Mambo muhimu yanayochangia kuharibika kwa maziwa Mihadhara Majadiliano Maswali & majibu Mbinu shirikishi za kufundisha watu wazima Aina ya vifaa vya kuhudumia & kuhifadhia maziwa Usafi na dawa za kusafi shia Namna ya kusafi sha vyombo vya maziwa - Kuangalia na kunusa - Alkoholi - Kuchemsha - Laktomita Saa 1 Saa 3 Saa 8Saa 7 Mihadhara Majadiliano Mafunzo ya mfano Mazoezi ya upimaji Majaribio ya mwisho ya mafunzo ya kinadharia (Dakika 30) na kwa vitendo (Saa 1) Cheti cha mafunzo ya msingi ya stadi za biashara ya maziwa bora Dakika 30 Dakika 30 Dakika 30 Dakika 30 Saa 1 4. Utunzaji na uhifadhi wa maziwa safi na salama Wafanyabiashara wadogowadogo wenye uzoefu na ujuzi katika stadi za utunzaji, uhifadhi na usafi rishaji Vyombo vilivyothibitishwa kuhifadhi maziwa Njia sahihi za kuhifadhi maziwa Utunzaji wa maziwa mahali pa kuuzia maziwa Mihadhara Majadiliano Mafunzo ya mfano Projekta Chatipindu Ubao Kalamu za mgandamizo Dakika 30 Dakika 30 Dakika 30 Saa 2